Leo tarehe
19 March ni sikukuu ya EID-EL-MAOLUD, sikuu ambayo waislamu
wenye imani duniani kote washerekeya kuzaliwa kwa nabii
Mouhammad.
Sherehe
hii ni sikukuu ambayo waislamu wenye imani husoma mchana hadi
usiku kitabau cha Korani takatifu, vitabu vya mfano wa maisha ya
nabii Muhammad na vitabu vingine vya kukuza imani ya
kiislamu,sherehe hii hutukia kila tarehe 12 ya mwezi wa Rabiul
Awwal, mwezi wa tatu wa kalenda ya kiisalamu.
Serekali
ya nigeria imetangaza siku ya leo kuwa siku ya mapumziko nchini
kote.
Imam
Fuad-adeyemi wa muskiti iitwayo Al habibiyah huko jijini Abuja
mji mkuu wa Nigeria alieleza kwa vyombo vya habari umuhimu wa
kusherekeya sikukuu ya leo , wanafunzi kadhaawa ma darasa za
elimu ya kiislamu walihotubia pia kuhusu sikuu ya leo na umuhimu
wake.
Eid-el-maulud inasherekewa Nigeria kwa njia za michezo kadhaa
,ikiwemo kutembea juu ya farasi na kubadilisha zawadi baina
waamini wengi wa kiislamu nchini kote nigeria.
Ofisi ya
huduma za raiya nchini Nigeria inayo julikana tena kwa jina la
DUE PROCESS imesema kwamba wa kontrakta waliopewa projeti ya
kukuza uduma za umeme nchini kote, itabidi irudishe kwa serekali
billioni 3.3 waliodai kutumia kwa kukuza huduma hizo
Kiongozi
wa ofisi hio Bwana EMEKA EZE, alishuhudia mbele ya tume la
wakilishi kwa huduma za moto wa umeme kwamba ofisi yake iliomba
fedha karibu billioni 150.6 za Naira, ila ofisi yake haikuelezwa
wakati malipo yale yalifanyika.
Bwana Eze
amesema tena kwamba hatua hio yakusikilizwa mbele ya tume la
bunge la taifa ni hatua muhimu sana , ikieleza kwamba maafisa
wote wasio julikana na raiya ya walio pokonya mali ya taifa,
faili zao zitafunuliwa mbele ya tume hilo kwa muda wa siku 60.
Wa seneti
nchini Nigeria wametangaza kuweka malipizi kali kwa watu wanao
husika, kwa kupotea angani kwa ndege la BEECHCRAFT, wakiwapa ma
saa 48 kwakuleta ripoti kama ndege hio imekwenda wapi.
Msimamizi
wa kamati ya seneti kwa huduma za safari ya anga, Chief Anyim
–Udeh aliye tangaza hayo alipokuwa akitoa ripoti kwa wa seneti
kuhusu kupotea kwa ndege hio hapo jijini Abuja.
Chief Udeh
ameeleza tena kuwa mambo yote sio barabara kabisa katika sekta
ya safari angani na akisema kuwa hatua uhimu zimechukuliwa sasa
kwa kutatua maswala yale.
Mwandishi
wetu Obiora Ani, ameripoti kwamba seneti imehakikisha uteuzi wa
watu 27 na msimamizi mpya wa tume lile.