Uchunguzi
 

Maandishi Matupu

Karibu Kwenye Idhaa Ya KiSwahili Ya Sauti Ya Nijeria.......................

COMORO

Kisiwa cha Anjouan kimetekwa masaa ma chache kiisha jeshi la Muungano wa Africa kuwasili kwakuunga mkono majeshi ya serekali kwaku mutimua coloneli muasi Mohamed  Bacar aliye chukua madaraka kisiwani humo mwezi wa Mei.

Kuchaguliwa kwake kama rais wa kisiwa cha anjouan mwaka jana kulitangazwa kama ni kinyume cha sheria ya serekali ya Comoro pamoja Umoja wa Afrika. 

Msemaji wa jeshi la Comoro Meja Ahmed Sidi akizugmuza kutoka kisiwa cha Moheli kilichon jirani na kile cha Anjouane, amesema kisiwa hicho hadi sasa kinakabidhiwa na jeshi la serekali. Ameongeza nakusema kuwa hadi sasa hakuna jeshi wa serekali ama ule wa  Muungano wa Afrika aliye uwaua ama kujehuriwa,

Na alihakikisha kwamba viongozi wa waasi wale walikimbia na hakuna aliyekamatwa hadi sasa. 

Awali maafisa wa Comoro walisema kundi la kwanza la wanajeshi 450 la Muungano wa Afrika liliingia usiku wakuamkia leo kutokea baharini na baadaye kidogo walifanikiwa na kuteka uwanja wa ndege wa Ouani na baadaye wakauteka mji wa Mustamudu. 

Milio ya bunduki na makombora mazito yalisikika wakati wanajeshi hao walipokua wakiingia mapema Alfajiri ya Juma nne. 

Wanajeshi wa Comoro wanasaidiwa na jeshi la Muungano wa Africa wanaofikia 1500 wakijimuisha wote kutoka Tanzania, Senegal na Sudan. 

Makamu rais wa serekali kuu amesema kwamba kiongozi huyo muasi atakamatwa nakupelekwa mahakamani kwa kujibu mashtaka ya uhalifu wa kivita.

MISRI

Maafifa wa usalama nchini Misri wametangaza kwamba mashua ya kivita ya Marekani imefungulia risasi boti ya wenyeji katika mfereji wa Suezi, nakusababisha kifo cha mtu mmoja wa wengine wawili kujeruhiwa vikali. 

Kikosi cha Marekani kimekusudia kufungua risasi kwa boti hio kiisha kuwaamuru wasi ijogeleye meli yao.

Meli hio ilikuwa na biashara ikiuza kwa meli zinazopita katika mfereji wa Suezi, ambako ni njia pia ya jeshi la Marekani. 

Meli hio ya kikosi cha Marekani ipo hapo ikitarajia kupewa ruhusa kupita bahari ya Mediteranea.

MUSUMBIJI 

Musumbiji na Ureno umeweka saini mkataba ya urafiki na usafiri, na nchi hizo zimerudia tena mkataba wao wa mwaka wa 1991 kwa kuondolea malipo kadhaa kwa raiya wao watapo safari katika chi hizo mbili. 

Hii ni hatua ya kwanza kwa Ureno kuanza uasiliano wa kiuchumi na nchi hio  ya ukoloni wake zamani, Rais Anibal Cavaco Silva yuko wizarani Musumbiji kwa muda wa siku tatu toka alipo wasili siku ya jumatatu kwa kukaza urafiki wa kiuchumi na wingine. 

Moja ya mkataba walio saini ni  matumizi ya liseni yakuendeza gari moja kwa nchi hizo mbili,ingawa pia majeshi ya Ureno yataleta mazoezi kwa wenzio wa Musumbiji. 

Nchi ya Musumbiji ilijipatia uhuru toka ukoloni wa Ureno mwakani 1975.

 
 

Home | Contact | VON | Contact Us | archive
Webmaster@voiceofnigeria.org :Change Password :VON Staff Sign Up
Copyright© 2007. All Rights Reserved Voice Of Nigeria. Developed by: VON ON-LINE

7255KHz 41m; 9690KHz 31m; 11770KHz 25m; 15120KHz  19m